Samatta anacheza soka Ubelgiji, hivi ni viwango vya mishahara vya wachezaji wa Ligi hiyo


Najua unatamani kujua maisha ya wanasoka wa Ubelgiji hususani katika kipindi hiki anachocheza 
soka mtanzania Mbwana Samatta nchini humo, kiukweli mshahara waSamatta haupo 
wazi katika vyombo vya habari, ila Ligi ya Ubelgiji wachezaji wanalipwa kwa mwezi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.epiphanTech.blogs.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara 
ya wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji ilikuwa inatajwa kuwa ya wastani wa euro 253,586
 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima.
Kwa mwezi huwa inatajwa kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania. Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa mwaka Anderlecht inalipa hadi  euro 600000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa mchezaji mmoja.
Klabu ya KRC Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wawww.epiphanTech.blogs.com, wachezaji wengi wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.
EURO elfu ishirini na tano ni zaidi ya milioni sitini za Kitanzania kwa sasa wakati Euro elfu 50 ni zaidi ya milioni mia moja ishirini za Kitanzania.
CHANZO CHA STORI: 
www.epiphanTech.blogs.com

No comments:

Post a Comment