NorthWest aanza kufundishwa muziki

NorthWest aanza kufundishwa muziki


NEW YORK, MAREKANI
MTOTO wa msanii wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West na mwanamitindo Kim Kardashian, North West, ameanza kufundishwa muziki.
Wazazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili wamedai kwamba ana kipaji cha hali ya juu na atakuja kuwa
msanii mzuri katika matumizi ya vifaa.
Kupitia akaunti ya Instagram, Kardashian aliiweka picha ya mtoto akiwa anajifunza muziki na kuanza kummwagia sifa.
“Siamini kuona mtoto mwenye kipaji kama hiki akiwa na umri mdogo, ninaamini tayari mwanangu atakuja kuwa nyota mkubwa katika muziki.
“Kwa kuwa amezaliwa katika familia ya watu maarufu basi ninaamini atakuja kuwa maarufu kama ilivyo sisi, sijui
kama atakuja kuwa kama mama yake juu ya urembo au atakuwa kama baba yake kufanya muziki, ila chochote
kinaweza kutokea,” aliandika Kardashian kwenye mtandao wa Instagram.
by Epiphan bernard.


1 comment: