Mwanamume ambaye alidanganya kuwa
kiwete aliyekuwa akitumia kiti cha magurudumu na ambaye alikuwa amefunga
dhahabu ya kilo 25 kwenye mapaja yake, amekamatwa kwenye uwanja wa
ndege nchini Bangladesh.
Dhahabu hiyo ya gharama ya dola milioni 1.5 ndiyo kubwa zaidi kukamatwa mwaka huu wakati Bangadesh ilibuka kuwa kituo cha kupitisha dhahabu kwenda nchini India.
Kupanda kwa kodi kwa dhahabu nchini India iliyo mnunuzi mkubwa zaidi wa dhahabu duniani kumechangia kuongezeka visa vya uiafarishaji wa dhahabu kwa njia haramu.
No comments:
Post a Comment