Mtu mwenye silaha ambaye aliwafyatulia risasi wabunge wa Republican wakati wakifanya mazoezi ya mchezo wa baseball mjini Washington DC ameuwa. Marekani
Kinara wa walio wengi bungeni Steve Scalise, ni mmoja wa wale waliojeruhiwa wakati wa kisa hicho cha mapema asubuhi katika hustani huko Alexandria , Virginia.
Mshambualiaji ambaye ni mzaliwa wa Illiois James T Hodgkinson, mwenye umri wa miaka 66, aliuawa baada ya ufyatulianaji wa risasi na polisi.
Waliojeruhiwa ni pamoja na polisi wawili.
Hodgkinson alikuwa amemfanyia kampeni mgombea urais wa Democratic Bernie Sanders.
Mbuge aliyepiwa risasi Steve Scalise |
Ukurasa wa Facebook ambao unaonekana kuwa wa Bwana Hodgkinsion, umejaa propaganda dhidi ya Republican na Trump.
Bwana Sanders ambaye ni Seneta wa Vermont amesema amehusunishwa na kitendo hicho cha Hodgkinson.
Rais wa Marekani Donald Trump ametaja shambulia hilo kuwa la kinyama.
Trump alimtembelea bwana Scalise ambaye alipiwa risasi kwenye nyonga na yuko hali mahuti baada ya kufanyiwa upasuaji.
Hospitali ilisema kuwa Bwana Scalise alivunjika mifupa, na kupata majeraha ya viungo vya ndani na hivyo atahitaji upasuaji zaidi.
No comments:
Post a Comment