Ashinda kesi ya kuitwa Zebra
Raia mmoja wa Austria ameshinda kesi ya kumwezesha kulibadilisha jina la familia yake na kuwa Zebra.
Mtu huyo alikata rufaa katika mahakama moja ya kikatiba nchini Austria baada ya mahakama moja ya chini kukataa pendekezo lake.
Babu yake jamaa huyo alibadili jina lake kutoka kwa Zebra 1950.
''Zebra limekuwa jina la familia kwa karne kadhaa kwa hivyo kulibadili imekuwa kinyume na sheria'' ,mahakama hiyo ya kikatiba imeamua.
Mahakama hiyo ya chini ilikuwa imeamua kuwa Zebra sio jina lililobuniwa nchini Austria.
Katika uamuzi huo wa mapema ,jaji alisema kuwa Zebra ni farasi anayeishi katika eneo la nyika.
Aliongezea kuwa majina mengine ya wanyama yangekubalika kwa kuwa yanatumika Austria kulingana na rekodi.
No comments:
Post a Comment