Kauli ya kwanza ya Suarez, baada ya kumaliza adhabu ya kumg’ata Chiellini na kujiunga na Uruguay.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay ambaye anaichezea klabu ya FC Barcelona yaHispania Luis Suarez amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu yake na kujiunga na kikosi cha timu yake ya taifa ya Uruguay kilichopo Montevideo.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 29 amejiunga na kikosi cha timu yake ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya michezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 dhidi yaBrazil na Peru.
Suarez alifungiwa kutoichezea Uruguay mechi 9 pamoja na kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi mwaka 2014 wakati wa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil, adhabu hiyo ilitolewa baada ya Luis Suarez kumg’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini kati mechi dhidi ya timu zao.
“Ni kweli nilifanya makosa nakubali, lakini hakukuwa na mantiki yoyote kwa mimi kufungiwa miezi minne kutojihusisha na soka, yaani hata kufanya mazoezi na klabu yangu, nilipewa adhabu kubwa kuliko hata kama ningekutwa nimefanya kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu” >>> Suarez

No comments:

Post a Comment